Waorthodoksi – Kanisa la Orthodox ╰⊰¸¸.•¨* Swahili

http://heavenonearthorthodoxy.wordpress.com

HEAVEN ON EARTH  – ORTHODOXY

Waorthodoksi – Kanisa la Orthodox

Waorthodoksi ni Wakristo wanaofuata mapokeo ya Mitume wa Yesu jinsi yalivyostawi kihistoria katika Ukristo wa Mashariki upande wa mashariki wa Dola la Roma iliyoitwa pia Bizanti na nje ya mipaka yake. Leo hii ni nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na nchi za Mashariki ya Kati.

Jina

Kanisa la Orthodoksi ni jina linalotumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya mitaguso saba ya kiekumeni tu. Leo, hasa kwa sababu ya uhamiaji, Kanisa la Orthodoksi lipo katika dunia nzima, likijumuisha watu milioni 200 hivi, lakini bado lina idadi kubwa ya waumini katika Ulaya ya Mashariki.

Jina hilo (“Orthodoksi”) lina asili ya Kigiriki likitokana na maneno “orthos”, yaani “nyofu”, “sahihi” na “doksa”, yaani “rai”, “fundisho” yaani “wenye fundisho sahihi”.

Jina hilo lilitungwa ili kutofautisha Wakristo waliofuata mafundisho rasmi ya imani yaliyotolewa na Mitaguso ya kiekumene dhidi ya mikondo mingine ya wakati ule.

Kwa namna ya pekee jina hilo lilitumika upande wa mashariki, hivi kwamba lilipotokea farakano la mwaka 1054, likabaki kama jina maalumu la makanisa yenye ushirika na Patriarki wa Konstantinopoli (leo Istanbul katika Uturuki).

Muundo

Makanisa ya kujitegemea ya Kiorthodoksi yanayotambuliwa na wote ni kama yafuatayo:

Upatriarki wa Konstantinopoli
Upatriarki wa Aleksandria
Upatriarki wa Antiokia
Upatriarki wa Yerusalemu
Upatriarki wa Moscow na Urusi
Upatriarki wa Peć na Serbia
Upatriarki wa Romania
Upatriarki wa Bulgaria
Upatriarki wa Georgia
Kanisa la Kiorthodoksi la Kipro
Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki
Kanisa la Kiorthodoksi la Poland
Kanisa la Kiorthodoksi la Albania
Kanisa la Kiorthodoksi la Ucheki na Slovakia

Makanisa mengine yaliyojitenga na hayo hayajakubalika.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s