Waorthodoksi – Kanisa la Orthodox ╰⊰¸¸.•¨* Swahili

http://heavenonearthorthodoxy.wordpress.com

HEAVEN ON EARTH  – ORTHODOXY

Waorthodoksi – Kanisa la Orthodox

Waorthodoksi ni Wakristo wanaofuata mapokeo ya Mitume wa Yesu jinsi yalivyostawi kihistoria katika Ukristo wa Mashariki upande wa mashariki wa Dola la Roma iliyoitwa pia Bizanti na nje ya mipaka yake. Leo hii ni nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na nchi za Mashariki ya Kati.

Jina

Kanisa la Orthodoksi ni jina linalotumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya mitaguso saba ya kiekumeni tu. Leo, hasa kwa sababu ya uhamiaji, Kanisa la Orthodoksi lipo katika dunia nzima, likijumuisha watu milioni 200 hivi, lakini bado lina idadi kubwa ya waumini katika Ulaya ya Mashariki.

Jina hilo (“Orthodoksi”) lina asili ya Kigiriki likitokana na maneno “orthos”, yaani “nyofu”, “sahihi” na “doksa”, yaani “rai”, “fundisho” yaani “wenye fundisho sahihi”.

Jina hilo lilitungwa ili kutofautisha Wakristo waliofuata mafundisho rasmi ya imani yaliyotolewa na Mitaguso ya kiekumene dhidi ya mikondo mingine ya wakati ule.

Kwa namna ya pekee jina hilo lilitumika upande wa mashariki, hivi kwamba lilipotokea farakano la mwaka 1054, likabaki kama jina maalumu la makanisa yenye ushirika na Patriarki wa Konstantinopoli (leo Istanbul katika Uturuki).

Muundo

Makanisa ya kujitegemea ya Kiorthodoksi yanayotambuliwa na wote ni kama yafuatayo:

Upatriarki wa Konstantinopoli
Upatriarki wa Aleksandria
Upatriarki wa Antiokia
Upatriarki wa Yerusalemu
Upatriarki wa Moscow na Urusi
Upatriarki wa Peć na Serbia
Upatriarki wa Romania
Upatriarki wa Bulgaria
Upatriarki wa Georgia
Kanisa la Kiorthodoksi la Kipro
Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki
Kanisa la Kiorthodoksi la Poland
Kanisa la Kiorthodoksi la Albania
Kanisa la Kiorthodoksi la Ucheki na Slovakia

Makanisa mengine yaliyojitenga na hayo hayajakubalika.

Mtakatifu Martino wa Tours, Ufaransa (+397) ╰⊰¸¸.•¨* Swahili

http//saintsofmyheart.wordpress.com

SAINTS OF MY HEART

baoba_tree_1.jpg

tumblr_mdt8114ntB1rz3pvd.jpg

Mtakatifu Martino wa Tours, Ufaransa

Mtakatifu Martino wa Tours, Ufaransa (+397)

Mtakatifu Martino wa Tours (Savaria, Panonia, leo Hungaria 316 – Candes-Saint-Martin, Gaul, leo Ufaransa 397) alikuwa mmonaki, halafu askofu (kuanzia 371 hadi kifo chake).

Alipokaribia kifo, walimuomba asiondoke, naye akasali hivi: “Ee Bwana, nikihitajiwa bado na watu wako, sikatai uchovu wa kazi: utakalo lifanyike!”

Maisha yake yaliandikwa na Sulpicius Severus yakawa kielelezo cha vitabu juu ya watakatifu.

Sifa yake ilienea haraka hivi kwamba aliheshimiwa kama mtakatifu ingawa hakuwa mfiadini kama kawaida ya wakati ule.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 8 Novemba.

Mtakatifu Moses wa Ethiopia (+405) – 28 Agosti ╰⊰¸¸.•¨* Swahili

http://saintsofmyheart.wordpress.com

SAINTS OF MY HEART

Mtakatifu Moses wa Ethiopia (+405)

28 Agosti

Musa Mwafrika, maarufu pia kama Musa Mwizi (330–405), alikuwa mmonaki padri nchini Misri na mmojawapo kati ya mababu wa jangwani.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai na tarehe 28 Agosti.

Mzaliwa wa Ethiopia, Musa alikuwa mtumishi wa afisa wa serikali nchini Misri mpaka alipofukuzwa kwa thuhuma za kuiba na kuua.

Akiwa jitu, akawa bosi wa kundi la majambazi lililotisha watu wa bonde la Nile kwa ukatili.

Alipojaribu kukwepa waliokuwa wanamwinda, alifichama kwa wamonaki wa jangwani huko Wadi El Natrun (Sketes), karibu na Alexandria. Juhudi za kiroho, utulivu na furaha walivyokuwa navyo vilimuathiri kwa dhati. Muda mfupi baadaye aliacha mtindo wake wa kuishi, akabatizwa na kujiunga na monasteri ile.

Kwanza alipata shida sana kuzoea nidhamu ya jumuia ile. Alipovamiwa na wezi chumbani mwake, aliwazidi nguvu akawaburuza hadi katika kikanisa walimokuwemo wenzake wakisali ili aambiwe awafanyie nini wageni hao.

Musa alikuwa na ari katika yote aliyoyafanya, lakini alikata tamaa alipojitambua si mkamilifu kutosha. Hapo abati Isidori alimchukua alfajiri hadi juu ya paa ili kutazama miali ya kwanza ya jua. Halafu akamuambia, “Taratibu tu miali ya jua inaondoa usiku na kuleta mchana mpya, na vilevile taratibu tu mtu anakuwa mwanasala kamili.”

Baadaye Musa akawa mwenyewe kiongozi wa jumuia ya wakaapweke katika sehemu nyingine ya jangwa akapewa upadrisho.

Alipokuwa na umri wa miaka 75 hivi, ilisikika kwamba kundi la Waberber limepanga kushambulia monasteri yao. Wenzake walitaka kujihami, lakini Musa aliwazuia akawaambia ni afadhali wakimbie kuliko kushika silaha. Mwenyewe na wengine 7 walibaki hadi walipouawa tarehe 1 Julai.

Kwa sababu hiyo Musa Mwafrika anaheshimiwa leo kama mtetezi wa msimamo wa kukataa silaha katika kudai haki.

Mt. Yohane Maximovitch wa Shanghai na San Francisco (+1966) – 2 Julai ╰⊰¸¸.•¨* Swahili

http://stjohnmaximovitchofsanfrancisco.wordpress.com

ST JOHN MAXIMOVITCH OF SAN FRANCISCO

Mt. Yohane Maximovitch

wa Shanghai na San Francisco (+1966)

2 Julai

Mt. Yohane Maximovitch wa Shanghai na San Francisco (Mikhail Borisovich Maximovitch; Adamovka, wilaya ya Izyum, mkoa wa Kharkov, leo nchini Ukraina, 4 Juni 1896 – Seattle, Washington, USA, 2 Julai 1966) alikuwa mmonaki, padri, askofu na mmisionari wa Kiorthodoksi huko China na Marekani.

Alijulikana pia kwa karama ya kutenda miujiza.

Alitangazwa na Kanisa lake kuwa mtakatifu tarehe 2 Julai 1994.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe hiyohiyo.

Link: Orthodox Christian Initiative for Africa

http://grforafrica.blogspot.com

Orthodox Christian Initiative for Africa

We are Orthodox Christian Greeks. Because we are Orthodox Christians, we love our country, our people and all the peoples of the earth; this of course includes our African brothers and sisters.

Link: Biblica – The Holy Bible in all languages

lonelyplanet-photographer-stuartbutler1974-caught-this-beautiful-moment-of-two-giraffes-sharing-a-1

http://www.biblica.com/en-us/bible/bible-versions/

Biblica

The Holy Bible in all languages

Sala ya Bwana (Lord’s Prayer – Pater Noster) ╰⊰¸¸.•¨* Swahili

https://africaofmyheart.wordpress.com

AFRICA OF MY HEART

baobab-ducks-000060800218_small.jpg

swahili-l.jpg

Sala ya Bwana

(Lord’s Prayer – Pater Noster)

Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu.
Utusamehe makosa yetu,
kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea.
Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.
Amin.